Kwenye ukoo wa BBM yangu nimeshuhudia marafiki kadhaa wakisema tumuombee mwigizaji Kajala kutokana na kilichompata ambapo nilipojaribu kufatilia baadhi ya marafiki zake wameniambia kilichompata.
Ni kwamba jana mchana Mrembo huyo ambae aliwahi kuwa mpenzi wa zamani wa producer P FUNK MAJANI amepelekwa kwenye gereza la SEGEREA Dar es salaam kutokana na kesi inayomkabili yeye na mume wake.
Rafiki wa karibu wa KAJALA mwigizaji SINTAH amesema “nilichosikia ni kwamba alikua kaolewa na mwanaume ambae ana kesi na TAKUKURU kwa kutumia hela vibaya”
Nilipopita kwenye djfetty.blogspot.com nimekutana na haya maelezo mengine kwamba Makosa mengine Katika kesi hiyo ya Kajala pamoja na mumewe Faraji Mchambo ni kula njama na kubadilisha umiliki wa nyumba pamoja na kutakatisha fedha haramu.
Wakili wa serikali Leonard Shayo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alidai kuwa Kajala na mumewe wameshitakiwa kwa kosa la kwanza la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote walitenda kosa hilo la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.
Shitaka la tatu walidaiwa Aprili 14 2010 huku wakijua ni kinyume na sheria walifanya kosa la kutakatisha fedha haram ambapo ni kosa lisilo na dhamana kisheria, Chambo hakuwepo mahakamani kwasababu yupo mahabusu kwa makosa mengine ambayo hayana dhamana yanayomkabili ya utakatishaji fedha.
Kajala alikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kwa uchungu mkubwa huku akilia pamoja na ndugu zake akiwamo mama yake aliyekuwepo mahakamani hapo huku Hakimu Fimbo akiahirisha kesi hiyo mpaka Aprili 20 mwaka huu ili kesi ije kwaajili ya kutajwa na pia kutolea maamuzi, maombi yaliyotolewa na wakili wa Alex Mgongolwa anayemtetea kajala
Posted by
Ngowi Grace
No comments:
Post a Comment