Wednesday, April 11, 2012

Rais Kikwete kufungua mkutano wa kimataifa wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa. 

                                                              
 POSTED BY JORAM JULIA BAPRM 12O16

 Rais Kikwete akifungua mkutano wa kimataifa wa mamlaka za kuzuia na kupambana na rushwa



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kufungua mkutano wa Kimataifa wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchi mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa na msemaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  Doreen Kapwani mjini Arusha na akasema kuwa hii ni mara ya kwanza mkutano wa namna hiyo kufanyika nchini ambapo zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kushiriki mkutano huo wa siku tatu.
Amezitaja baadhi ya nchi zizotarajia kushiriki kwenye mkutano huo kuwa ni Morocco, Uingereza, Qatar, Uganda, Romania, Brazil, Austria, India, Belgium, Spain, Ukraine, Malsiyia, Namibia na Mwenyeji Tanzania.
Kwapwani amesema kuwa mkutano unafanyika hapa nchini wakati Tanzania imepata heshima kubwa ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri juu ya Rushwa ya Umoja wa Afrika Machi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment