Junior ni mmoja wa wababe wanaoupaisha mchezo huu hasa kutokana na mitindo pamoja na mbinu anazotumia kusaka ushindi mbele ya wababe wengine licha ya kuwa na umbo dogo.
Ray Mysterio Junior alizaliwa mnamo mwaka 1974 Desemba 12 mjini CHULA VISTA,CALIFORNIA,MAREKANI.Akiwa anaitwa OSCAR GUTIERREZ,wazazi wake wote wanaasili ya Mexico.Sasa hivi Ray anaishi katika jiji la San Diego,CalforniaMnamo mwaka 2002 aliamua kuondoa neno JUNIOR katika jina lake la awali ikiwa ni siku chache baada ya kujiunga na kamisheni ya WWE. na kumfanya atambulike kama Ray Mysterio.
Ilikuwa ni mwaka 1992 mjini Mexico City,Mexico bwana mdogo huyu alikuwa katika matembezi yake,aliona police wakimfuatilia ndipo alipoanza kukimbiza gari yake kwa kasi sana,kiasi cha kusababisha ajali,ambapo aligonga gari ndogo iliyokuwa mbele yake.Bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa kwenye ajali ile,ndipo ilishuka mijibaba yenye miraba minne na kuanza kumshambulia Ray kwa kipigo.Kumbe mwili si kigezo wala kipimo cha uwezo,bwana mdogo huyo aliweza kuwachakaza vibaya sana watu wale hatimaye wakakimbia na kumwacha Mysterio akikamatwa na police,baada ya upekuzi ikagundulika kuwa Ray hakuwa na makosa kwa kile kilichomfanya atimue mbio na gari baada ya kuhisiwa amebeba madawa ya kulevya.
Alikuwa ni Ray Misterio Sir mdau mkubwa sana wa mieleka, ambaye ni mjomba wake na Ray alipoamua kumhamasisha pamoja na kumfundisha juu ya mchezo huo na ndipo alipoamua kumsajili kwenye kamisheni ya Extreme Championship Wrestiling{ECW}.mapema mwaka 1995.
Kijana huyo mwenye urefu wa futi 5 nchi 6 na uzito wa kilo 175 ndiye aliyekuwa bingwa wa msimu wa 2010/2011 anayetambuliwa na kamisheni inayosimamia mchezo huo wa WWE kwenye uzito wa Raw and Smackdown alioupata baada ya kumshida RANDY ORTON ingawa pambano hilo liliingiwa dosari baada ya kundi la Mysterio kuingia uwanjani na kuvuruga utaratibu.
Japo mieleka ni moja ya burudani nzuri sana ambayo umaarufu wake unakua kila kukicha ulimwenguni kote baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Tanzania watu wamekuwa na imani haba juu ya ukweli wa mchezo huo hasa wanapoona nguvu na aina ya mapigo ya mchezo huo jukwaani.Lakini ukweli unabaki kuwa huu ni mchezo kama ilivyo mpira wa miguu.
juma mayasa 12029 .
No comments:
Post a Comment