APRIL 30, 2012
KISA CHA MKWELIMA NA MSHENGA KTK ANGA ZA UKWENI
Jamaa mmoja toka pande za nyanda za juu kusini mwa Bongoland aliambatana na mshenga wake kwenda kupeleka posa.Ilipotimu muda wa maakuli jamaa aliungua baada ya kuwa amefakamia beche a.k.a kipunga bila kuwa na full stop wala comma mdomoni mwake,seuze semi colon.Baada ya kuungua mshenga akafunguka kama ifuatavyo:-
Mshenga,"kama umeungua tema"
Mkwelima akajibu, "niteme chakula?"
Mshenga akaendelea,"kama uwezi tema, meza"
Mkwelima akasema,"nimeze moto"
Mshenga akahitimisha,"kunywa maji"
Mkwelima akang'aka,"ninywe maji niondoe radha ya chakula"
Kama ingelikuwa wewe ndio mkwelima(jembe) ungelifanya nini?Toa maoni yako
See u next time!
By Oyaro jr
No comments:
Post a Comment