Monday, April 30, 2012

A GIRL KILLED HERSELF THROUGH SOCIAL MEDIA

Binti aliyejiua kupitia mtandao wa kijamii(myspace)

Binti wa miaka 13 barani Uropa ameripotiwa kujinyonga kufutia kukataliwa na mpenzi wake kupitia mtandao wa kijamii(myspace). Binti huyo kwa jina la Megan Meir alikataliwa na mpenzi wake kwa jina Josh, miaka 16, ambaye hawakuwahi kukutana uso kwa uso isipokuwa kupitia online relationship. 

Wiki sita baada  ya kifo cha binti huyo wazazi wake walibaini kuwa Joash alikuwa mpenzi "feki" wa kutengeneza. Josh ni jina lilibuniwa na baba mtu mzima ambaye ni jirani wa kairbu na marehemu kupitia msaada wa binti yao aliyekuwa rafiki wa kairbu wa Megan. 

Wenye kutafuta wapenzi pitia social media mpo hapo!


By Oyaro jr

NOTICE TO GROUP NINE MEMBERS

You are all informed that on wednesday of May, 2012 after the session of PR and Law, we are going to have a meeting concerning the farewell party of the group. The venue is Facebook garden.The main agenda in farewell paty.

Don't miss!
Your contribution is your presense!



Hyera Delistas
Communication Officer
Group Nine BAPRM 3

CLIMB MOUNT KILIMANJARO FOR LOWER COST

Attention SAUT students!

For those who are interested to climb mount Kilimanjaro for a lower cost are advised to contact mr. Nguma Reginald, BAPRM three by using the contact below. The has been working with Big Expedition Safaris, a tourism organization in Arusha.

Contacts:
Phone: 0756 441000

Sunday, April 29, 2012

APRIL 30, 2012

KISA CHA MKWELIMA NA MSHENGA KTK ANGA ZA UKWENI

Jamaa mmoja toka pande za nyanda za juu kusini mwa Bongoland aliambatana na mshenga wake kwenda kupeleka posa.Ilipotimu muda wa maakuli jamaa aliungua baada ya kuwa amefakamia beche a.k.a kipunga bila kuwa na full stop wala comma mdomoni mwake,seuze semi colon.Baada ya kuungua mshenga akafunguka kama ifuatavyo:-

Mshenga,"kama umeungua tema"

Mkwelima akajibu, "niteme chakula?"

Mshenga akaendelea,"kama uwezi tema, meza"

Mkwelima akasema,"nimeze moto"

Mshenga akahitimisha,"kunywa maji"

Mkwelima akang'aka,"ninywe maji niondoe radha ya chakula"

Kama ingelikuwa wewe ndio mkwelima(jembe) ungelifanya nini?Toa maoni yako




See u next time!
By Oyaro jr



Tuesday, April 24, 2012


Tanzania: Taifa la ombaomba hadi michezoni


by juma mayasa 12029
Ni msamiati wa kawaida sana katika medani ya michezo nyumbani Tanzania; kutembeza bakuli! Maana yake hapa ni kuwa ombaomba.

Baada ya serikali yetu kuwa kinara wa kutembeza bakuli kwa wahisani, sasa michezo nayo imefuzu katika kufuata nyayo; kutembeza bakuli

Ipo mifano kadhaa walau ya hivi karibuni. Chama cha Mpira wa Pete Tanzania (Chaneta) kinajiandaa kwa Mashindano ya Afrika. Tayari bakuli limeanza kutembea kila kona likibisha mlango wa maskini na tajiri kuomba mchango. Bila bakuli, mashindano hakuna na timu yetu haitashiriki

Timu niipendayo kuliko zote Tanzania, timu ya soka ya taifa ya wanawake (Twiga Stars), nao wanatembezewa bakuli hivi sasa wakijiandaa na mashindano yaliyo mbele yao. Kwao Twiga Stars kutembezewa bakuli limekuwa ni jambo la kawaida.

Twende kwenye kikapu. Huko ni kichefuchefu zaidi! Timu za kikapu za jiji la Dar es Salaam (Dream Teams) zinajiandaa na mashindano ya majiji (Inter-Cities) ambayo mwaka huu yatafanyika nchini Uganda.

Ukata umetanda kambini, wachezaji wanakwenda mazoezini kwa pesa yao mfukoni, kila mchezaji na vifaa vyake, na haijulikani kama nauli ya Kampala itapatikana au la, achilia mbali posho. Bakuli linatembezwa sasa

Timu ambayo imekuwa nyanya kila siku lakini yenye bahati ya kupata ufadhili mnono katika miaka mitano iliyopita, Taifa Stars, mara kadhaa pamoja na udhamini wake imekuwa ikikosa kupata huduma kadhaa muhimu ikiwemo kuweka kambi kwa muda wa kutosha, kuwaita wachezaji wote wanaosakata gozi nje na kuwalipa posho stahiki, ama kuweka kambi katika hoteli yenye hadhi na sababu imekuwa ikidaiwa kuwa ni ukata
Timu ya taifa ya ndondi inalia ukata, karate na Tae Kwon Do mambo ni hayo hayo. Mpira wa mikono, wavu na magongo sidhani hata kama inaendelea tena kuchezwa Tanzania, kama ipo basi timu zote zitakuwa za majeshi.

Kwa ujumla hakuna penye ahueni, kila siku na kila mchezo ni ukata kwa kwenda mbele na suluhisho pekee Kwa viongozi wetu wa michezo, ni kutembeza bakuli.

Lakini siwalaumu sana viongozi wetu wa michezo kwa kutegemea mabakuli na kuwa omba omba kama �Matonya� kila siku. Ni ka-utamaduni walikokarithi kutoka kwenye serikali yetu ambayo laiti tungekuwa na mashindano ya kimataifa ya kutembeza mabakuli, basi Tanzania ingetwaa dhahabu kila mwaka! Na sasa maji yanafuata mkondo.

Ukiona tabia hii imeota mizizi katika sekta yoyote ile, tambua kuwa hapo kupata maendeleo ni sawa na ngamia kupenya mwenye tundu la sindano. Tusahau maendeleo iwe kwenye ndondi, riadha, soka, netiboli au kikapu kwa mchezo huu wa kutegemea mabakuli.

Lakini jambo la kujiuliza, hivi kweli hakuna njia mbadala ya kuepuka tabia hii ya kujiaibisha kila siku kugonga milango ya watu na kuomba? Mimi naamini njia mbadala zipo, tena nyingi, lakini mawazo mgando ya viongozi wa michezo Tanzania ndiyo sababu ya kupenda kuendekeza aibu hii.

Chama cha Mpira wa Kikapu mkoani Dar es Salaam kwa miaka mingi ligi yake ilikuwa ikidhaminiwa na bia ya Kilimanjaro. Tangu jamaa hao wajiondoe, basi akili za viongozi wote wa BD zikawa zimeganda na wameshindwa kutafuta udhamini ama kupata njia ya kujitegemea hadi leo.

Nakumbuka wakati ule kikapu kikiwa kikapu cha ukweli, enzi za akina Patrick Nyembera wa Pazi na akina Lotty Cheyo wa Vijana, nilikuwa nalipa fedha kuingia uwanjani kuangalia mechi, na Uwanja wa Ndani wa Taifa ulikuwa unajaa kwelikweli.

Leo hii hakuna hata kiingilio na uwanjani hakuna watazamaji tena, mvuto umepotea kwa viongozi kukosa ubunifu wa kuuendeleza mchezo.

Enzi zile wakati netiboli inachezewa kwenye uwanja uliofunikwa na mabati wa Relwe Gerezani nikiwa shule ya msingi hadi sekondani, nilikuwa natoka Mabibo hadi Relwe Gerezani kuhakikisha naingia kuangalia mechi kama sio �kupiga chabo� kwenye matundu ya mabati uwanjani hapo. Netboli ilikuwa netiboli kweli. Leo hii ovyooooo

Chaneta imebaki kutimuana, kugombana na Chaneza na kuwa ombaomba wa kutupwa badala ya kutafuta mbinu za kujitegemea na kuvutia wadhamini.

Vivyo hivyo, kwa michezo mingine niliyoitaja hapo juu, hakuna uliosalimika iwe soka, ngumi, riadha, wavu, mikono, baiskeli na mingineyo.

Hivi kweli tutarajie maendeleo katika michezo nchini Tanzania kwa kutembeza mabakuli?
Jahazi la michezo Tanzania linazamishwa na viongozi wanaokosa ubunifu kama tulio nao sasa. Bila kuhakikisha viongozi hawa wanasafishwa wote bila kusalia hata mmoja, tusitarajie maendeleo ya aina yoyote katika michezo.

Tutarajie ubia baina ya wanamichezo na ombaomba Matonya kuendelea kushika kasi kila kukicha. Kupata maendeleo michezoni kwa umatonya wetu wa kutembeza mabakuli, ni kuota ndoto za alinacha!
          

HAYA NDIYO WANAYOFANYA WENZETU KUKUZA VIPAJI



 Planning permission has finally been given for 10 football pitches – four of which will be floodlit – a new pavilion and a 119-space car park to be built on land off Cawston Road, as part of a scheme that will also see 250 homes built on the site.
And sporting campaigners are urging the community to show their support for the project as they now have to raise £500,000 of match funding to ensure it is completed.
The plans suffered delays when rival developers tried to get them overturned ,but after Broadland District Council gave them the final nod of approval last month, it allowed work to begin in earnest.
The sports ground will become home to Aylsham Football Club, which desperately needs space as it continues to grow, host St Giles Cricket Club and could become a centre of excellence for coaching.
But it is planned to cater for more than just sport as talks are also being held with the local Scout groups and the pavilion will be available for private hire.
As part of the planning permission developer Youngs Farms is donating £500,000 to kickstart the project and fundraising is now being planned to bring in the rest of the cash that will see it home.
Ian Potter, Aylsham FC chairman, said he was “really pleased” the plans had been given the green light but despite the celebrations the hard work was just beginning.
“We have created a number of events to raise money but also to raise the profile of what we’re doing for the community. Ultimately we can only do this with the support of the people who are part of the club, part of the cricket club and people in the community,” he added. “If we don’t raise the money we’ll
miss the opportunity.”
A trust is now being established, which will be responsible for the gifted cash, and once up and running members will also start to apply for grants to boost the project’s coffers.
The money is expected to be handed over by the summer and construction work started as soon as possible, with the sports ground ready for play by 2014. Building work on the homes is anticipated to begin next year and take around 50 months to complete through four phases.
Aylsham FC has been working for four years with the Norfolk Football Association to source extra pitches for its 17 teams as the facilities it currently uses - spread over two sites at the town “rec” and high school - have “stifled its growth”.
Gavin Lemmon, development manager at Norfolk FA, added to Mr Potter’s call for the community to get behind the scheme.
He said: “With planning permission now in place it’s really been the impetus the club needed to be able to rally their members. But it’s not the case they’re going to get this all through grant aid, they’re going to have to do traditional fundraising.
“The facility is for the community and the community needs to demonstrate they want the project to be a success.”
The club already has several fundraising events planned, including a match between Aylsham and a team of Norwich City all stars later this month, but Mr Potter said campaigners were “desperate” for more people to help with the fundraising drive.
                                                                           JUMA  MAYASA     12029